Tarehe 12.08.2012 kilifanyika kikao cha walimu
wakuu wote wa eneo la Cluster ya Buhigwe na Waratibu Elimu Kata na Mratibu wa
kituo cha walimu Bhigwe.Jumla ya walimu wakuu 33 na waratibu elimu kata 12 na
mratibu Trc walihudhuria kikao hicho. Kikao hicho kilifanya tathmini ya mtihani
wa utimilifu wa Cluster ya buhigwe na mambo mengine yanayohusu elimu. Yafuatayo
ni yatokanayo na kikao hicho
Washiriki walikubaliana wanunue photocopy
machine itakayotumiwa na shule zote hasa katika shule za mitihani , hivyo
ilikubaliwa kila shule ichangie shilingi 32,000/= ili kuweza kutimiza sh
2,100,000/= kwaajili ya manunuzi ya Photocopy machine. Fedha hiyo inatakiwa
hadi kufikia january 2014 iwe imekusanywa. Pia tulikubaliana kuanza kituo cha
walimu kianze kutoa mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa walimu wanaojiendeleza
katika vipindi vya likizo. Pia walimu wakuu walikubaliana kuwa wanachangia
shilingi 7000 kila mwaka kwa ajili ya malipo ya mlinzi wa kituo cha walimu
Buhigwe. Pia kiwango cha uchangiaji kwa ajili ya mtihani wa utimilifu wa TRC
kilipandishwa toka sh 3000/= hadi sh 4000/=.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni