Andalio la somo: Ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia
unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika kwa darasa fulani./ ni dira
ya kumwongoza mwalimu wakati wa kufundisha.
Umuhimu wa andalio la somo.
Huonyesha wazi malengo ambayo mwalimu anatarajia yafikiwe na mwanafunziwake wakati wa kipindi.
Humwongoza mwakimu kufundisha kwa hatua anapokuwa darasani.
Humwonyeshab mwalimu vitendo vya kufanya wakati wa ujifunzaji na ufundishaji.
Vipengele vya andalio la somo
Chati itakayoonyesha taarifa za awali , Tarehe, darasa, kipindi/somo, muda,idadi ya wanafunzi waliopo na wasiopo.
Ujuzi : ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge
mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na
mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi.
Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na
ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Mada na mada mada ndogo : Hizi ni mada kuu na mada ndogo ambazo zimeonyeshwa kwenye muhtasati wa somo.
Lengo kuu: Ni lengo la jumla ambalo mwalimu anatarajia wanafunzi wake kulifikia katika ufundishajina ujifunzaji.
Malengo mahsusi: lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha
ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba
vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu
vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua,
kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango
vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k
kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake
cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Jedwali linaonyesha hatua za ufundishaji.
- utangulizi: Utangulizi ndio hatua ya kwanza ya somo, mada unayotaka
kufundisha haipo mbali sana na maisha ya mwanafunzi, ni vema kama
mwalimu ukaanza mada yako kwa kutafuta maarifa ya awali aliyonayo
mwanafunzi.
Ni vema kufahamu wanafunzi wana maarifa na uzoefu gani kuhusu kile
utakachokwenda kukifundisha.Lengo ni kuanza kwa kile wanachokifahamu
wanafunzi kisha kuelekea kile kipya, Kwa hiyo kile kile wanachokifahamu
kitakuwa ni msingi mzuri ambao kile kipya watakachojifunza kitaleta
ujuzi. Mfano unaweza ukatumia njia ya bungua bongo, maswali na majibu au
changanya kete kutafuta maarifa ya awali kwa mwanafunzi.
- Ujuzi mpya: Katika hatua hii Mwalimu anahitaji kufikiri kwa kina
kuhusu stadi na maarifa atakayotumia mwanafunzi katika kujenga ujuzi
unaotarajiwa. i.e Kuwaongoza wanafunzi kufanya
vitendo mbalimbali vilivyopo kwenye vitendo vya ujifunzaji ili kuweza kujenga maarifa mapya.
-Kuimarisha maarifa: Katika hatua hii inampasa mwalimu kuwashirikisha
wanafunzi katika kuunganisha maarifa waliyojifunza ili kuwe na
mshikamano wa dhana husika.
- Tafakuri : Mwalimu uwaongoze wanafunzi wako kutafakari jinsi
maarifa waliojifunza yanavyohusiana na maisha yao na ujuzi wanaotarajiwa
kuujenga. Vilevile kupima ufanisi au udhaifu wa ujifunzaji na
ufundishaji.
-Hitimisho: Mwalimu tafuta njia mbalimbali za kuhitimisha somo lako,
mfano kutumia maswali yanayohitaji majibu mafupimafuipi kwa kile
walichojifunza, kumhitaji kila mwanafunzi kubainisha dhana muhimu
alizojifunza.
- Vitendo vya upimaji, Ni tendo linalifanyika mfululizo toka mwanzo
hadi mwisho wa somo. Ni ukweli kwamba utakuwa umeandaa vitendo vya
kupima kila hatua ya mada yako. Lakini kuna uwezekano wa kubadili
vitendo vya upimaji kulingana na jinsi somo linavyoendelea.
-Tathmini: Tathmini inahusu ufanisi wa somo unaotokana na matokeo ya
vitendo vya upimaji katika mfululizo wa hatua nzote za somo. Tathmini
ya mwanafunzi inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ujifunzaji Mfano
mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo , ni mambo gani
mmeyapenda katika hii mada, mambo gani hamkuyapenda, na uwaagize watoe
sababu kwa majibu waliyoyatoa, mnahitaji msaada gani ili muelewe zaidi?
Au wagawie vikaratasi waandike maoni yao kuhusu mada iliyofundishwa na
tathmini ya mwalimu inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ufundishaji,
Tafakari ya matokeo ya upimaji uliofanya katika hatua zote za somo na
matokeo ya tathmini ya mwanafunzi.
-Maoni: Maoni yanatolewa baada ya tathmini, Mwalimu atabainisha mambo
yatakayowezesha kuboresha ujifunzaji wa somo. Mfano, kwa wale ambao
hawakuweza kufikia ujuzi uliotarajiwa utatumia mbinu gani kuwasaidia, au
maoni /ushauri kuhusu namna ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji
wako.
Muundo wa andalio la somo.
TAREHE
DARASA
KIPINDI
MUDA
IDADI YA WANAFUNZI
IDADI YA WANAFUNZI
IDADIWALIOHUDHURIA
IDADI YA WALIOANDIKISHWA
ME
KE
JML
ME
KE
JML
Ujuzi…………………………
Mada kuu………………………………………
Mada ndogo…………………………………..
Lengo kuu……………………………………….
Lengo mahsusi……………………………..
Zana/vifaa:…………………………………………..
Rejea:…………………………………………….
Hatua za somo
Tarehe
Vitendo vya ufundishaji
Vitendo ufundishaji
Vitendo ujifunzaji
utangulizi
Ujuzi mpya
Kuimarisha maarifa
Tafakuri
Hitimisho
Tathmini ta wanafunzi…………………………………………..
Tathmini ya mwalimu…………………………………………….
Maoni
nomba unisaidie rejea za haya machapisho tafadhari. ubarikiwe sana
JibuFutaNaomba kuoneshwa mfano wa vitendo vya upimaji
JibuFutaJe, mwanafunzi ameweza.... Kwaisahihi?
FutaOnesheni jinsi gani andalio la somo la mtaala mpya linavyojazwa!
JibuFuta