Jumapili, 11 Agosti 2013

Walimu wafeli mitihani vibaya

  Hakuna daraja la kwanza kwa vyuo vyote
  Watalazimika kurudia mtihani kufikia viwango
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
Wakati serikali ikisuasua kutoa ripoti ya tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyokuwa ikichunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, matokeo ya mtihani wa ualimu ya mwaka huu nayo ni janga.

Katika matokeo ya mtihani wa ualimu waliofanya Mei mwaka huu ambayo yametolewa jana na Baraza la Mtihani la Taifa (Necta), wahitimu 2,906 wa ngazi ya stashahada wanatakiwa kurudia mitihani (supplementary) ndani ya miaka miwili huku wengine 533 wakiwa wamefeli kwa daraja la 0.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa kwenye tovuti ya Necta na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini, yanaonyesha kwamba hakuna kabisa mhitimu aliyefaulu kwa kiwango cha juu (distinction), 27 wamefaulu kwa daraja pili (credit) na waliofaulu kwa daraja tatu (pass) ni 6,374.

Madaraja ya mitihani huo yamepangwa kwa distinction (sawa na daraja la kwanza), credit (sawa na daraja la pili), pass (sawa na daraja la tatu), supplementary (kurudia baadhi ya masomo) na fail (daraja sifuri)Jumla ya vyuo 139 vilifanya mtihani huo, kati yake vya astashahada ni 90 na stashahada ni 49.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo kama Mpwapwa yenye wahitimu 442 ni mhitimu mmoja tu aliyepata daraja pili yaani credit wakati waliofaulu kwa daraja tatu yaani pass ni 295, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 136 na waliofeli ni tisa.

Chuo cha Marangu chenye wahitimu 1,026 daraja pili ni 7, la tatu ni 630, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 343 wakati waliopata daraja 0 ni 38. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba chuo cha Monduli waliopata daraja pili ni 9, la tatu ni 295, wanaorudia ni 66 na 0 ni wawili.

Chuo cha Korogwe kati ya wahitimu 1,080 matokeo yanaonyesha kwamba hakuna waliopata daraja la pili, la tatu ni 655, wanaorudia ni 328 na 0 ni 77 wakati Eckenforde hakuna pia aliyepata daraja la pili, wakati daraja la tatu 51, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo vya Arusha, Mtwara, Benjamin Mkapa, Dakawa, Butimba, Chuo cha Ualimu Zanzibar, Pemba Islamic na Bukoba Lutheran hakuna waliopata daraja pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Pemba Islamic waliopata daraja la tatu ni wanne, wanaorudia ni 29 na 0 ni 19; wakati Chuo cha Ualimu Zanzibar daraja la tatu ni sita, wanaorudia ni 31 na 0 ni 16 wakati Bukoba Lutheran daraja la tatu ni 12, wanaorudia ni wanne na waliopata 0 ni watatu.

Dakawa waliofaulu kwa daraja la tatu ni 352, wanaorudia ni 124 na 0 ni 24; Mtwara daraja la tatu ni 304, wanaorudia ni 145 na 0 ni 27; Benjamin Mkapa daraja la tatu ni watano, wanaorudia ni saba na 0 ni wawili; Arusha daraja la tatu ni 14, wanaorudia ni wanane na 0 ni saba wakati Butimba daraja la tatu ni 497, wanaorudia ni 283 na 0 ni 18.

Klerruu wahitimu 227 waliofaulu kwa daraja pili ni wawili, daraja la tatu ni 175, wanaorudia ni 39 na 0 ni saba; Patandi la pili ni mmoja, daraja la tatu ni 60, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16; Bunda hakuna hata mmoja aliyepata C, wakati daraja la tatu ni 313, wanaorudia ni 159 na 0 ni 23 wakati Morogoro mmoja amefaulu kwa daraja pili, 665 wamefaulu kwa daraja la tatu ni 274 wanarudia na 49 wanamepata 0.

Tukuyu hakuna daraja la pili na 445 wamepata daraja la tatu, 107 wanarudia wakati 12 wamepata 0. Kasulu hakuna daraja la pili, 204 wamepata daraja la tatu, wanaorudia ni 77 na 0 ni 14 wakati St. Mary’s hakuna waliopata daraja la pili wala wanaorudia, daraja la tatu ni watano na 0 ni mmoja.

Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa katika vyuo vyote kwa ngazi ya cheti (Grade A) yaani astashahada, wahitimu 5,608 wamefaulu kwa daraja pili wakati waliopata daraja la tatu ni 17,339. Pia wapo 207 waliopata 0.

Matokeo yaliyopo kwenye tovuti hiyo ni ya jumla ya vyuo 86 vya ngazi ya astashahada ya ualimu, elimu maalum vinne, stashahada (diploma) ya ualimu vyuo 48 na kimoja cha ufundi.
SOURCE: NIPASHE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni