Na Robert Mihayo, Dar Es Salaam
Katiba, ni msingi wa sheria na sera zote
za nchi husika. Hivyo ni nadra kubadilika
mara kwa mara. Lakini huweza
kubadilishwa pale jamii inapoona
umuhimu wa kufanya hivyo kwa nia ya
kuiboresha.
Sasa hivi watanzania tunajadili mchakato
utakaotumika katika kuibadili katiba ya
nchi yetu. Wananchi wamekuwa
wakihamasishwa kuitumia fursa hii vizuri
ili muda wa kutoa mapendekezo ya katiba
mpya utakapofika, waweze kuleta
mapendekezo yatakayoboresha maisha
yao kutokana na kuwa na katiba bora.
Ni dhahiri kuwa kuna maeneo mengi
yanayohitaji kuboreshwa. Moja ya
maeneo hayo ni sekta ya elimu ambayo
ndiyo nguzo mama ya sekta nyingine zote
zikiwemo uchumi, afya, kilimo, sheria,
jamii na kadhalika.
Elimu ndiyo njia pekee inayowezesha
nchi kujenga raslimali watu ili kupambana
na adui umasikini, kuboresha afya na
katika kujenga nchi yenye uchumi imara
Kupitia mipango ya Maendeleo ya Elimu
ya Msingi (MMEM) na wa Sekondari
(MMES), mnamo mwaka 2010, idadi ya
shule za msingi ilipanda kutoka 11,873
mnamo mwaka 2001 hadi 15,816 wakati
idadi ya watoto walioandikishwa
iliongezeka takribani mara mbili kutoka
4,875,185 mwaka 2001 to 8,419,305
mwaka jana, 2010.
Idadi ya shule za sekondari pia imepanda
sana kutoka shule za sekondari 937
mwaka 2001 hadi shule 4,266 mwaka
2010; ikiwa ni ongezeko la 355%! Kila
kata ina walau shule moja ya sekondari!
Wakati idadi ya wanafunzi 638,699
walioandikishwa katika shule za
sekondari mwaka 2010, mwaka 2001 ni
wan a f u n z i 2 8 9 , 6 9 9 t u n d io
walioandikishwa. Kwa hakika haya siyo
mafanikio ya kubeza kwani hakuna nchi
ambayo imeweza kupiga hatua za
maendeleo kwa kuendelea kutotoa vijana
wanaoelea katika bahari ya ujinga!
Tatizo ni kuwa upanuzi huu wa elimu ya
msingi na sekondari hauendi sambamba
na malengo yanayobainishwa katika Sera
ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995
ambayo ni pamoja na kuwaandaa
wanafunzi kujiunga na ulimwengu wa
kazi, kumwezesha kila mtoto kupata
mbinu za kupata njia za kutatua matatizo,
kujenga uwezo wa kujifunza, uwezo wa
kujiamini na kujiendeleza katika masuala
ya sayansi na teknolojia n.k.
Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka
2008 ulionesha kuwa, “Ingawa shule
nyingi zimejengwa na walimu wengi zaidi
kuajiriwa, na wanafunzi wengi
kuandikishwa …ubora wa elimu
haujaimarika sana.” Pia Shirika la Uwezo,
limebaini kuwa kati ya wanafunzi 10
wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi
watatu hawawezi kufanya hesabu za
darasa la pili. Aidha, takribani mhitimu
mmoja wa elimu ya msingi kati ya
wahitimu watano, hawezi kusoma hata
Kiswahili cha darasa la pili.
Kwa kifupi ni kuwa uwezo wa wanafunzi
kusoma, kuhesabu, kuandika, kuongea,
kujenga hoja, kujiamini, kuwa wabunifu
umezidi kupungua kadri siku zinavyopita.
Matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne
mwaka 2010 yalionesha kuwa ni asilimia
12 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani
huo ndio waliofaulu kwa kiwango cha
Divisheni 1 hadi 3! Karibu nusu ya
watahiniwa walipata divisheni 0; na
asilimia 88% walipata divisheni 4 na 0.
Shule zilizoongoza kwa kufanya vibaya ni
shule za kata ambako ndiko watoto wa
walalahoi wamesheheni. Ni dhahiri kuwa
kuna kasoro kubwa katika mfumo wa
elimu yetu.
Enzi za Mwalimu, kulikuwa na Sera ya
Ujamaa na Kujitegemea. Katiba ya
mwaka 1977, ilitamka wazi kwamba kila
mtu alikuwa ana haki ya kuelimishwa na
kila mtu alikuwa na uhuru wa kutafuta
elimu katika fani aipendayo kwa uwezo
na upeo wake.
Hivyo mtoto wa mkulima masikini
aliweza kusoma darasa moja na mtoto wa
Hakimu wa Tarafa hiyo; na kama
angechaguliwa kwenda shule ya
sekondari angeweza kusoma darasa moja
na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au
hata wa Rais na kushirikiana nao katika
hali ya usawa kabisa!
Wakati huo, Serikali iligharamia elimu
kwa kutumia kodi za wananchi. Elimu
ilikuwa ni mojawapo ya huduma za jamii.
Mwalimu Nyerere alipenda kila mtoto
apate elimu bora itakayomwezesha
k u k a b i l i a n a n a c h a n g amo t o
atakazokumbana nazo katika maisha yake
na ya jamii yake.
Lakini baada ya kuingia masoko huria,
sera zilibadilika na kuwataka watu
“wachangie” katika uendeshaji wa elimu,
kile kifungu cha katiba kilibadilishwa na
kusomeka; “Kila mtu anayo haki ya
kujielimisha, …” Yaani watu walipe kodi,
lakini watumie kipato chao kidogo,
kulipia huduma za jamii, hii ni sawa na
kulipa kodi mara mbili! Katiba mpya
inayokuja lazima ifute sera hii, kwa kuwa
inaligawa taifa.
Tofauti na enzi za Mwalimu ambapo
watoto wote walikuwa na haki ya kupata
elimu bora itakayowasaidia katika maisha
yao na jamii zao, sasa elimu bora
inatolewa kwa watoto wa matajiri, watoto
wa walalahoi hawana fursa hiyo tena. Hii
imejenga matabaka ya walio nacho na
wasionacho.
Kwa mfano shule zenye vifaa muhimu
vya kufundishia na walimu wa kutosha ni
za gharama kubwa; hivyo wanaoweza
kusomesha watoto wao huko ni matajiri
tu. Shule za serikali na kata ambazo
zinatoa elimu kwa gharama nafuu
ambako ndiko watoto wa masikini
wamerundikana, hazina vifaa kama
maabara, maktaba, vitabu wala walimu
bora au wa kutosha, madarasa
yamefurika. Idadi kubwa ya watoto
waliofanya vibaya katika mtihani wa
Kidato cha 4 ni wale waliokuwa
wakisoma katika shule za kata ambazo ni
viota vya kutotoa watoto wanaopata
elimu ambayo haitawasaidia lolote
maishani mwao wala ya jamii zao.
Wakati umasikini unazidi kuwaelemea
watanzania wengi, shule zinazotoa elimu
bora zinazidi kuwa za gharama kubwa!
Tofauti na enzi za Mwalimu, elimu sasa si
huduma ya jamii bali ipo kibiashara zaidi.
Mathalani, ada ya kumusomesha mtoto
kwa mwaka mmoja katika baadhi ya shule
hizi ni zaidi ya ada anayolipa mwanafunzi
anayesomea shahada ya uzamili pale
Mlimani! Sera za kibaguzi za aina hii
zinaligawa taifa. Katiba ijayo ifute
ubaguzi wa aina hi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni