Jumatano, 7 Agosti 2013

TUKO TAYARI NA 'BIG RESULTS NOW' YA RAIS KIKWETE?

President Jakaya Kikwete
Rais Kikwete akizungumza katika mkutano huo nchini Malaysia

Agosti 3,2013- Jumamosi.
Na Oscar Sabutoke:
 HIVI karibuni Tanzania imezindua Mpango 'Big Results Now' maana yake mpango wa 'tekeleza sasa kwa matokeo makubwa'. Mpango huu unalenga kuboresha maeneo makuu matano ambayo ni afya, elimu,gesi na nishati, uchukuzi na kilimo.
Maeneo haya yamechukuliwa kama ndiyo chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini kwa miaka ijayo.  Sote tunatambua hili halikuwa wazo letu binafsi ni mpango ambao tumeunakili toka Malaysia na hata serikali imekiri kuwa imekopa mawazo kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Programu ambacho kipo chini ya Ofisi ya Rais wa Malaysia kijuliknacho kama Pemandu.

 Kwa lugha ya kiingereza ni kwamba,'Under the initiative, the government commits to adopt and customise the Malaysian ‘Big Fast results’ known as Performance Management & Delivery Unit (PEMANDU) to design and implement model to suit local operations.'

Bila shaka taarifa hizi ziliwafikia Watanzania  kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali.Natambua haikuwa kazi rahisi kunakili hii programu kutoka kwenye mtandao au kwenye kitabu.  Jopo la viongozi na maafisa wa wizara mbalimbali walikwenda Malaysia kwa lengo la kujifunza zaidi kuhusu programu hii na wakarudi na mawazo ambayo yalionekana yanafaa kufanyiwa kazi na kundi dogo la wataalamu mbalimbali lilikutana hoteli ya white sand kwenye maabara ya uchambuzi ili kututengenezea programu yetu ya Fast Big Results Now.

Maandalizi haya yote yametumia fedha za walipa kodi na ni dhahili kwamba lazima tupate matokeo chanya yenye thamani ya fedha zilizotumika kwenye mpango huo.    Bado najiuliza maswali kadhaa, juhudi zimefanyika sawa, fedha zimeanza kutumika na zitaendelea kutumika, lakini tunaweza kufanya kama walivyofanya wenzetu kule Malaysia? Nilijiuliza kwa sababu tayari msimamizi mkuu wa programu hii ameshateuliwa na ameanza kazi, lakini lakini kuna kila dalili kwamba hata hii programu haitafanikisha kufika popote.  Siku zote tumekuwa na mbwembwe nyingi za kubuni majina ya miradi isiyozaa matunda! kwani iko wapi Kilimo Kwanza?
 Kwanini nasema hivi? Nimejaribu kutafuta hata hii programu name kama Mtanzania japo noisome niielewe maudhui na mkakati wa hii programu, lakini sijapata.

Nilitaraji kitu kikubwa kama hiki ambacho Watanzania wanapaswa kukifahamu kwa kina wangewekewa kwenye maktaba za taifa au website, wakajua serikali inataka kufanya nini, na kwa wakati gani kuhusu hayo maeneo yaliyobainishwa ili na wao washiriki katika kuyafikia malengo hayo kwani bila kuwashirikisha wananchi tangu hatua za awali serikali peke yake haiwezi kutekeleza programu hii.

Tunashukuru hata Profesa Muhongo Waziri wa Nishati na Madini aliweza kuitisha mdahalo uliojumuisha wadau mbalimbali ikiwapo jopo la watendaji walioapa kufanya kazi kwa uaminifu na kuweka rehani nyadhifa zao, waliapa iwapo wananchi watabaini utendaji hafifu  wawaondoe madarakani.
 Nadhani hata hii programu nayo ni siri japo inawahusu Watanzania wote katika hatua za kuitekeleza. Wenzetu Malaysia kabla ya kufanya chochote waliamua kubainisha nini maana ya neno mabadiliko. Kwa wenzetu Malaysia ilikuwa rahisi sana. Neno mabadiliko walisema ni 'kubadilika tofauti na ufanyavyo sasa'.

Walifanya tathmini na kugundua kuwa mfumo wao haukuwa sahihi na haukuwa wazi, viongozi hawakuwajibika ipasavyo, hawakujituma kufanya kazi, hawakuwa na Uzalendo  na hawakupenda kupata matokeo makubwa.   Haya yote waliyabaini na wakayafanyia kazi na ndiyo maana leo tumeona mafanikio yao na tumethubutu kunakili programu yao.

Nauliza tuko tayari kufanya kama walivyofanya Malaysia kuajiri watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwenye Pemandu, watu wenye ujuzi stahili na wenye bidii ya kufanya kazi bila hata kulipwa fedha za muda wa ziada kazi (overtime)?
Sisi hapa tumezoea kufanya kikao lazima posho, kufanya kazi zaidi lazima posho.Je tuko tayari kufanya kazi kwa bidii hata kama hatulipwi posho? Tuko tayari kuachana na ile staili ya mjomba nimlete au kamleta mjomba wetu na tujikite kuajiri watu ambao ni wabunifu na wenye uwezo wa hali ya juu kubaini changamoto na kuzitolea ufafanuzi na kuzitatua?

Ukimuuliza Idrisa Jalla ambye ndiye Mtendaji Mkuu wa Pemandu hata kupitia Tweeter yake atakueleza siri ya mafanikio. Moja anabainisha wazi kuwa wamejikita sana kuifanya Pemandu iwe kwenye mfumo wa sekta binafsi yaani licha ya kwamba ni kuboresha huduma au mambo mbalimbali, lakini mawazo yao yako kama vile nao wanapaswa kuzalisha faida na wako kwenye ushindani na kampuni nyingine kuwa nani atatatua zaidi matatizo ya Wamalaysia kwa haraka zaidi.

Je tuko tayari kuwa na haya mawazo waliyonayo kina Idris Jalla na wenzake ndani ya Pemandu?
Mheshimiwa Jakaya Kikwete amesema viongozi watapimwa kwa matokeo na utendaji wao. Je tuko tayari kuwawajibisha wale wazembe wasiowajibika kwa maslahi ya Watanzania ili tufanye kama wafanyavyo Malaysia?
Kwa historia ya nchi yetu kazi nyingi za serikali wanaziita Permanent and Pensionable na kwa kuwa hawako kiushindani suala la kumfukuza kazi mtu kwa kushindwa kupata matokeo tarajiwa ni ngumu sana. Je yuko tayari kuwafukuza na kubadili mikataba isiwe ya kudumu na kujali zaidikipato tena ili mtu asipofanya kazi aondolewe moja kwa moja na siyo kubadilishwa kitengo?

'Toa maoni yako hapa, tujadili kwa pamoja na BUHIGWETRC 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni