Jumamosi, 17 Agosti 2013

Katiba ijayo ifute ubaguzi wa aina hii.

Na Robert Mihayo, Dar Es Salaam
Katiba, ni msingi wa sheria na sera zote
za nchi husika. Hivyo ni nadra kubadilika
mara kwa mara. Lakini huweza
kubadilishwa pale jamii inapoona
umuhimu wa kufanya hivyo kwa nia ya
kuiboresha.
Sasa hivi watanzania tunajadili mchakato
utakaotumika katika kuibadili katiba ya
nchi yetu. Wananchi wamekuwa
wakihamasishwa kuitumia fursa hii vizuri
ili muda wa kutoa mapendekezo ya katiba
mpya utakapofika, waweze kuleta
mapendekezo yatakayoboresha maisha
yao kutokana na kuwa na katiba bora.
Ni dhahiri kuwa kuna maeneo mengi
yanayohitaji kuboreshwa. Moja ya
maeneo hayo ni sekta ya elimu ambayo
ndiyo nguzo mama ya sekta nyingine zote
zikiwemo uchumi, afya, kilimo, sheria,
jamii na kadhalika.
Elimu ndiyo njia pekee inayowezesha
nchi kujenga raslimali watu ili kupambana
na adui umasikini, kuboresha afya na
katika kujenga nchi yenye uchumi imara
Kupitia mipango ya Maendeleo ya Elimu
ya Msingi (MMEM) na wa Sekondari
(MMES), mnamo mwaka 2010, idadi ya
shule za msingi ilipanda kutoka 11,873
mnamo mwaka 2001 hadi 15,816 wakati
idadi ya watoto walioandikishwa
iliongezeka takribani mara mbili kutoka
4,875,185 mwaka 2001 to 8,419,305
mwaka jana, 2010.
Idadi ya shule za sekondari pia imepanda
sana kutoka shule za sekondari 937
mwaka 2001 hadi shule 4,266 mwaka
2010; ikiwa ni ongezeko la 355%! Kila
kata ina walau shule moja ya sekondari!
Wakati idadi ya wanafunzi 638,699
walioandikishwa katika shule za
sekondari mwaka 2010, mwaka 2001 ni
wan a f u n z i 2 8 9 , 6 9 9 t u n d io
walioandikishwa. Kwa hakika haya siyo
mafanikio ya kubeza kwani hakuna nchi
ambayo imeweza kupiga hatua za
maendeleo kwa kuendelea kutotoa vijana
wanaoelea katika bahari ya ujinga!
Tatizo ni kuwa upanuzi huu wa elimu ya
msingi na sekondari hauendi sambamba
na malengo yanayobainishwa katika Sera
ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995
ambayo ni pamoja na kuwaandaa
wanafunzi kujiunga na ulimwengu wa
kazi, kumwezesha kila mtoto kupata
mbinu za kupata njia za kutatua matatizo,
kujenga uwezo wa kujifunza, uwezo wa
kujiamini na kujiendeleza katika masuala
ya sayansi na teknolojia n.k.
Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka
2008 ulionesha kuwa, “Ingawa shule
nyingi zimejengwa na walimu wengi zaidi
kuajiriwa, na wanafunzi wengi
kuandikishwa …ubora wa elimu
haujaimarika sana.” Pia Shirika la Uwezo,
limebaini kuwa kati ya wanafunzi 10
wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi
watatu hawawezi kufanya hesabu za
darasa la pili. Aidha, takribani mhitimu
mmoja wa elimu ya msingi kati ya
wahitimu watano, hawezi kusoma hata
Kiswahili cha darasa la pili.
Kwa kifupi ni kuwa uwezo wa wanafunzi
kusoma, kuhesabu, kuandika, kuongea,
kujenga hoja, kujiamini, kuwa wabunifu
umezidi kupungua kadri siku zinavyopita.
Matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne
mwaka 2010 yalionesha kuwa ni asilimia
12 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani
huo ndio waliofaulu kwa kiwango cha
Divisheni 1 hadi 3! Karibu nusu ya
watahiniwa walipata divisheni 0; na
asilimia 88% walipata divisheni 4 na 0.
Shule zilizoongoza kwa kufanya vibaya ni
shule za kata ambako ndiko watoto wa
walalahoi wamesheheni. Ni dhahiri kuwa
kuna kasoro kubwa katika mfumo wa
elimu yetu.
Enzi za Mwalimu, kulikuwa na Sera ya
Ujamaa na Kujitegemea. Katiba ya
mwaka 1977, ilitamka wazi kwamba kila
mtu alikuwa ana haki ya kuelimishwa na
kila mtu alikuwa na uhuru wa kutafuta
elimu katika fani aipendayo kwa uwezo
na upeo wake.
Hivyo mtoto wa mkulima masikini
aliweza kusoma darasa moja na mtoto wa
Hakimu wa Tarafa hiyo; na kama
angechaguliwa kwenda shule ya
sekondari angeweza kusoma darasa moja
na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au
hata wa Rais na kushirikiana nao katika
hali ya usawa kabisa!
Wakati huo, Serikali iligharamia elimu
kwa kutumia kodi za wananchi. Elimu
ilikuwa ni mojawapo ya huduma za jamii.
Mwalimu Nyerere alipenda kila mtoto
apate elimu bora itakayomwezesha
k u k a b i l i a n a n a c h a n g amo t o
atakazokumbana nazo katika maisha yake
na ya jamii yake.
Lakini baada ya kuingia masoko huria,
sera zilibadilika na kuwataka watu
“wachangie” katika uendeshaji wa elimu,
kile kifungu cha katiba kilibadilishwa na
kusomeka; “Kila mtu anayo haki ya
kujielimisha, …” Yaani watu walipe kodi,
lakini watumie kipato chao kidogo,
kulipia huduma za jamii, hii ni sawa na
kulipa kodi mara mbili! Katiba mpya
inayokuja lazima ifute sera hii, kwa kuwa
inaligawa taifa.
Tofauti na enzi za Mwalimu ambapo
watoto wote walikuwa na haki ya kupata
elimu bora itakayowasaidia katika maisha
yao na jamii zao, sasa elimu bora
inatolewa kwa watoto wa matajiri, watoto
wa walalahoi hawana fursa hiyo tena. Hii
imejenga matabaka ya walio nacho na
wasionacho.
Kwa mfano shule zenye vifaa muhimu
vya kufundishia na walimu wa kutosha ni
za gharama kubwa; hivyo wanaoweza
kusomesha watoto wao huko ni matajiri
tu. Shule za serikali na kata ambazo
zinatoa elimu kwa gharama nafuu
ambako ndiko watoto wa masikini
wamerundikana, hazina vifaa kama
maabara, maktaba, vitabu wala walimu
bora au wa kutosha, madarasa
yamefurika. Idadi kubwa ya watoto
waliofanya vibaya katika mtihani wa
Kidato cha 4 ni wale waliokuwa
wakisoma katika shule za kata ambazo ni
viota vya kutotoa watoto wanaopata
elimu ambayo haitawasaidia lolote
maishani mwao wala ya jamii zao.
Wakati umasikini unazidi kuwaelemea
watanzania wengi, shule zinazotoa elimu
bora zinazidi kuwa za gharama kubwa!
Tofauti na enzi za Mwalimu, elimu sasa si
huduma ya jamii bali ipo kibiashara zaidi.
Mathalani, ada ya kumusomesha mtoto
kwa mwaka mmoja katika baadhi ya shule
hizi ni zaidi ya ada anayolipa mwanafunzi
anayesomea shahada ya uzamili pale
Mlimani! Sera za kibaguzi za aina hii
zinaligawa taifa. Katiba ijayo ifute
ubaguzi wa aina hi

MAADA

5.1 Muundo na Hali za Maada
17
Muda: Saa 5
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha muundo wa maada.
b) Kuainisha hali tatu za maada.
c) Kufanya majaribio ya kuhusianisha muundo na hali za maada
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Majadiliano katika vikundi kubainisha muundo wa maada.
b) Kutumia maswali na majibu kubainisha muundo wa maada na kuainisha hali
tatu za maada.
c) Kutumia ramani ya dhana kuainisha hali tatu za maada.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chati inayoonyesha hali tatu za maada.
b) Barafu, maji, jiwe, kiberiti na jiko.
c) Sufuria au beseni
Upimaji
a) Insha na zoezi.
b) Orodha hakiki.
5.2 Mabadiliko ya Maada
Muda: Saa 5
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kuaridhia mabadiliko ya kiumbo na kikemikali ya maada.
b) Kufanya majaribio ya kuonyesha mabadiliko ya kiumbo na kikemikali.
c) Kutofautisha badiliko la kiumbo na kikemikali.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bungua bongo
b) Majadiliano katika vikundi
c) Onyesho mbinu kuonyesha mabadiliko ya kiumbo na kikemikali ya
maada.
d) Uchunguzi wa kubaini badiliko la kiumbo na kikemikali.
18
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chumvi, sukari,
b) barafu, maji,
c) moto, mshumaa, kiberiti,
d) sodium kaboneti na riboni ya magnesiam na neli jaribio.
Upimaji
a) Mazoezi .
b) Mkoba wa kazi.
c) Fomu ya uchunguzi

UFUNDISHAJI MADA YA NISHATI

Na Oscar Sabutoke

4.1 Nishati Endelevu
Muda: Saa 6
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubaini vyanzo endelevu vya nishati.
b) Kuaridhia namna maji, upepo na jua vinavyotumika kuzalisha nishati.
c) Kutengeneza modeli za:
(i) Paneli za kuvuna nishati ya jua
(ii) Kuvuna nishati ya upepo na maji.
(iii) Gurudumu na mota
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Mchoro wa Venn
b) Fikiri-jozisha-wasilisha kubaini vyanzo endelevu vya nishati.
c) Onyesho mbinu kuaridhia namna vinu vya upepo na maji na paneli
zinavyoweza kuzalisha nishati.
d) Kufanya ziara ya mafunzo kubaini namna nishati anuwai
zinavyozalishwa.
13
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Modeli za paneli za kuvunia nishati ya jua.
b) Modeli za kinu upepo, maji na jenereta.
Upimaji
a) Kazi mradi ya kutengeneza modeli za kinu upepo, maji na
jenereta.
b) Insha
4.2 Nishati ya Sauti
Muda: Saa 6
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza vyanzo vya sauti.
b) Kuaridhia namna sauti inavyosafiri.
c) Kuelezea dhana ya mwangwi, namna unavyotokea na jinsi ya
kuudhibiti.
d) Kutengeneza vifani vya ala za muziki.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bungua bongo.
b) Jaribio la kamba inavyoweza kutengeneza mawimbi.
c) Uchunguzi jinsi mawimbi ya maji yanavyosafiri toka chanzo na
yanavyorudi nyuma yakigonga kizuizi.
d) Ziara ya kutembelea sehemu zinazoweza kuakisi sauti na kufanya
vitendo vyenye kusababisha mwangwi kutokea
e) Kazi mradi kutengeneza ala za muziki.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Ngoma, Filimbi, Zeze, Marimba
b) Kamba
c) Uzi
14
d) Dishi lenye maji na jiwe
e) Mazingira yenye kuweza kufanya mwangwi.
f) Upimaji
g) Kazi mradi
h) Insha ya kuelezea juu ya kutengeneza chumba cha mkutano
kisichoruhusu mwangwi kutokea.
i) Mkoba wa kazi
4.3 Nishati ya Sumaku
Muda: Saa 6
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza sifa na kanuni za sumaku.
b) Kuchora mistari ya kani za sumaku.
c) Kueleza matumizi ya sumaku.
d) Kuaridhia jinsi nishati ya sumaku inavyoweza kutumika kuzalisha
nishati ya umeme.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bungua bongo
b) Majaribio yenye kuonyesha kuvutana na kukwepana kwa ncha za
sumaku.
c) Kufanya jaribio kuonyesha mistari ya kani za sumaku.
d) Kufanya ziara penye vinu vya kufua umeme.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Miche ya sumaku, dainamo ya baiskeli na mota
b) Misumari, vipande vya chuma, unga wa chuma.
c) Spika ya redio na kipaza sauti.
Upimaji
a) Zoezi
b) Testi
15
c) Insha kuhusu nishati ya sumaku inavyoweza kugeuzwa kuwa
nishati ya umeme.
4.4 Nishati ya Umeme
Muda: Saa 6
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kuainisha vyanzo vya umeme.
b) Kuaridhia njia za umeme na vifaa vinavyohusika.
c) Kuunda sakiti mfuatano na sakiti sambamba.
d) Kueleza dhana ya mkondo, volteji na ukinzani.
e) Kukokotoa ukinzani, mkondo na volteji katika sakiti ya umeme.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Maswali na majibu.
b) Kutumia onyesho mbinu katika kuunda sakiti mfuatano na sakiti
sambamba.
c) Kutumia mbinu ya onesho mbinu juu ya dhana na ukokotoaji wa
mkondo, ukinzani na volteji katika sakiti ya umeme.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chati zinazoonyesha vyanzo vya umeme, njia na vifaa
vinavyohusika.
b) Betri/seli, balbu/glopu, swichi, amita, voltimita, nyaya za
kuunganishia sakiti.
Upimaji
a) Insha
b) Majaribio juu ya ukokotoaji wa mkondo, ukinzani na volteji katika
sakiti ya umeme.
c) Kazi mradi ya kuunda sakiti mfuatano na sakiti sambamba.
4.5 Nishati ya Mwanga
Muda: Saa 6
16
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubaini vyanzo vya mwanga.
b) Kueleza sifa na tabia za mwanga.
c) Kuaridhia kuakisiwa kwa mwanga kwenye vioo bapa, mbonyeo na
mbinuko.
d) Kuaridhia kupinda kwa mwanga katika media zenye densiti tofauti.
e) Kuelezea matumizi ya kuakisiwa na kupinda kwa mwanga.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Kutumia changanyakete katika vikundi kubaini vyanzo, sifa na
tabia za mwanga.
b) Kutumia onyesho mbinu kuaridhia kuakisiwa kwa mwanga
kwenye vioo bapa, mbonyeo na mbinuko na kuaridhia kupinda
kwa mwanga katika media zenye densiti tofauti.
c) Maswali na majibu.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chati zinazoonyesha vyanzo asili na visivyo asili vya mwanga.
b) Kurunzi mshumaa, kitabu, kibatari, chati ya mazigazi, vioo, glasi,
chupa, maji na prizimu.
Upimaji
a) Insha
b) Uwasilishaji kuhusu matumizi ya kuakisiwa na kupinda kwa
mwanga.
c) Kazi mradi kuaridhia kupinda kwa mwanga katika media zenye
densiti tofauti.

KUMBUKUMBU ZA SOMO/SHAJARA LA SOMO.

KUMBUKUMBU ZA SOMO/SHAJARA LA SOMO.
Ni muhtasari unaotayarishwa na mwalimu wa somo kuonyesha mada kuu na mada ndogo alizofundisha,wakati alipofundisha, na jina au sahihi yake. Pamoja na kumbukumbu hii, mwalimu ana kumbukumbu zingine zinazotumika kama rejea za kazi alizofanya. Mfano nukuu za somo, andalio la somo, azimio la kazi.
Umuhimu wa kumbukumbu za somo.
Huonyesha mambo yaliyofundishwa na wakati yalipofundishwa.
Mwalimu huweza kupima kiasi cha mada alizokwisha kufundisha kwa kulinganisha na azimio la kazi.
Humwelekeza mwalimu mpya mahali pa kuanzia.
Huweza kupima muda uliotumika katika ufundishaji wa mada ukilinganisha na azimio la kazi.
MUUNDO WA SHAJARA LA SOMO
MWEZI
Wiki
MADA KUU
MADA NDOGO
TAREHE
KUANZA
TAREHE
KUMALIZA
MADA ZILIZOFUNDISHWA
SAHIHI NA MAONI YA MWALIMU WA SOMO
SAHIHI NA MAONI YA MKUU WA IDARA.
SAHIIHI NA MAONI YA MKUU WA SHULE
Jan

ANDALIO LA SOMO

Andalio la somo: Ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika kwa darasa fulani./ ni dira ya kumwongoza mwalimu wakati wa kufundisha.
Umuhimu wa andalio la somo.
Huonyesha wazi malengo ambayo mwalimu anatarajia yafikiwe na mwanafunziwake wakati wa kipindi.
Humwongoza mwakimu kufundisha kwa hatua anapokuwa darasani.
Humwonyeshab mwalimu vitendo vya kufanya wakati wa ujifunzaji na ufundishaji.
Vipengele vya andalio la somo
Chati itakayoonyesha taarifa za awali , Tarehe, darasa, kipindi/somo, muda,idadi ya wanafunzi waliopo na wasiopo.
Ujuzi : ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Mada na mada mada ndogo : Hizi ni mada kuu na mada ndogo ambazo zimeonyeshwa kwenye muhtasati wa somo.
Lengo kuu: Ni lengo la jumla ambalo mwalimu anatarajia wanafunzi wake kulifikia katika ufundishajina ujifunzaji.
Malengo mahsusi: lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Jedwali linaonyesha hatua za ufundishaji.
- utangulizi: Utangulizi ndio hatua ya kwanza ya somo, mada unayotaka kufundisha haipo mbali sana na maisha ya mwanafunzi, ni vema kama mwalimu ukaanza mada yako kwa kutafuta maarifa ya awali aliyonayo mwanafunzi.
Ni vema kufahamu wanafunzi wana maarifa na uzoefu gani kuhusu kile utakachokwenda kukifundisha.Lengo ni kuanza kwa kile wanachokifahamu wanafunzi kisha kuelekea kile kipya, Kwa hiyo kile kile wanachokifahamu kitakuwa ni msingi mzuri ambao kile kipya watakachojifunza kitaleta ujuzi. Mfano unaweza ukatumia njia ya bungua bongo, maswali na majibu au changanya kete kutafuta maarifa ya awali kwa mwanafunzi.
- Ujuzi mpya: Katika hatua hii Mwalimu anahitaji kufikiri kwa kina kuhusu stadi na maarifa atakayotumia mwanafunzi katika kujenga ujuzi unaotarajiwa. i.e Kuwaongoza wanafunzi kufanya
vitendo mbalimbali vilivyopo kwenye vitendo vya ujifunzaji ili kuweza kujenga maarifa mapya.
-Kuimarisha maarifa: Katika hatua hii inampasa mwalimu kuwashirikisha wanafunzi katika kuunganisha maarifa waliyojifunza ili kuwe na mshikamano wa dhana husika.
- Tafakuri : Mwalimu uwaongoze wanafunzi wako kutafakari jinsi maarifa waliojifunza yanavyohusiana na maisha yao na ujuzi wanaotarajiwa kuujenga. Vilevile kupima ufanisi au udhaifu wa ujifunzaji na ufundishaji.
-Hitimisho: Mwalimu tafuta njia mbalimbali za kuhitimisha somo lako, mfano kutumia maswali yanayohitaji majibu mafupimafuipi kwa kile walichojifunza, kumhitaji kila mwanafunzi kubainisha dhana muhimu alizojifunza.
- Vitendo vya upimaji, Ni tendo linalifanyika mfululizo toka mwanzo hadi mwisho wa somo. Ni ukweli kwamba utakuwa umeandaa vitendo vya kupima kila hatua ya mada yako. Lakini kuna uwezekano wa kubadili vitendo vya upimaji kulingana na jinsi somo linavyoendelea.
-Tathmini: Tathmini inahusu ufanisi wa somo unaotokana na matokeo ya vitendo vya upimaji katika mfululizo wa hatua nzote za somo. Tathmini ya mwanafunzi inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ujifunzaji Mfano mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo , ni mambo gani mmeyapenda katika hii mada, mambo gani hamkuyapenda, na uwaagize watoe sababu kwa majibu waliyoyatoa, mnahitaji msaada gani ili muelewe zaidi? Au wagawie vikaratasi waandike maoni yao kuhusu mada iliyofundishwa na tathmini ya mwalimu inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ufundishaji, Tafakari ya matokeo ya upimaji uliofanya katika hatua zote za somo na matokeo ya tathmini ya mwanafunzi.
-Maoni: Maoni yanatolewa baada ya tathmini, Mwalimu atabainisha mambo yatakayowezesha kuboresha ujifunzaji wa somo. Mfano, kwa wale ambao hawakuweza kufikia ujuzi uliotarajiwa utatumia mbinu gani kuwasaidia, au maoni /ushauri kuhusu namna ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wako.
Muundo wa andalio la somo.
TAREHE
DARASA
KIPINDI
MUDA
IDADI YA WANAFUNZI
IDADI YA WANAFUNZI
IDADIWALIOHUDHURIA
IDADI YA WALIOANDIKISHWA
ME
KE
JML
ME
KE
JML
Ujuzi…………………………
Mada kuu………………………………………
Mada ndogo…………………………………..
Lengo kuu……………………………………….
Lengo mahsusi……………………………..
Zana/vifaa:…………………………………………..
Rejea:…………………………………………….
Hatua za somo
Tarehe
Vitendo vya ufundishaji
Vitendo ufundishaji
Vitendo ujifunzaji
utangulizi
Ujuzi mpya
Kuimarisha maarifa
Tafakuri
Hitimisho
Tathmini ta wanafunzi…………………………………………..
Tathmini ya mwalimu…………………………………………….
Maoni

AZIMIO LA KAZI



AZIMIO LA KAZI
Ni mpangilio au utaratibu unaomwezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo na kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki , mwezi, na muhula.Ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani.
Umuhimu wa azimio la kazi
Humsaidia mwalimu kwenda na mtiririko mzuri wa mada.
Humwonyesha mwalimu muda wa kufundisha kila mada.
Huonyesha zana/vifaa/njia ya kumsaidia mwalimu katika ufundishaji wake.
Kuonyesha malengo ya ufundishaji wa somo hilo katika muda aliopanga.
Wakati wa kuandaa andalio la somo kuna mambo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa,
Kuangalia kalenda au ratiba ya shule ambayo itakuongoza katika kuandaa azimio lako la kazi kwa kigezo cha muda.
Kusoma kwa makini muhtasari wa somo la kiswahili na kuweza kubaini mada, malengo , zana, na ujuzi ambao utatakiwa wanafunzi wako waupate katika mada husika.
Kuhakikisha kwamba vifaa vya muhtasari, vipo na vinatosheleza mfano, vitabu vya kiada, vitabu vya ziada, kiongozi cha mwalimu, kitabu cha mwalimu, na kitabu cha mwanafunzi.
VIPENGELE VYA AZIMIO LA KAZI
Ujuzi ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Katika kusoma ujuzi uliopo katika muhtasari wa somo la kiswahili , inakupasa kujua ujuzi ni upi, na maudhui ni yapi, kwani ujuzi huohuo huweza kujengwa na maudhui mengine.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Malengo mahsusi lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Sifa za malengo mahsusi : – Ni lazima libebe kitendo kinachopimika wakati unapofundisha.
– Malengo yahusiane na kiwango cha uwezo wa mwanafunzi.
– Muda wa malengo utajwe waziwazi
– Kiwango cha kufikia kila lengo kiwezeshwe.
– Kipindi kimoja kisiwe na malengo mengi.
Mwezi na Wiki Katika kugawa muda unatakiwa kuzingatia idadi ya vitendo vitakavyofanyika ili mwanafunzi ajenge ujuzi. Kuna baadhi ya vitendo vinahitaji muda mrefu na vingine vinahitaji muda mfupi kukamilika.
Vipindi Idadi ya vipindi itazingatia na uzito na wigi wa vitendo katika mada husika. Jiulize vitendo vya kiwango cha juu vina uzito sawa na vitendo vya kuchunguza? Katika muhtasari umepewa muda wa idadi ya ya jumla ya vipindi kwa mada kuu, hakikisha kuwa umevigawa kwa uwiano sawa kulingana na vitendo.
Vitendo vya Ufundishaji Kumbuka unapoandika vitendo vya ujifunzaji wewe ni mwezeshaji/wewe ni msaada kwa mwanafunzi wako katika utendaji wake. Katika kuandika vitendo nya ufundishaji unatakiwa kuonyesha yale matendo yote utakayoyafanya mwalimu pamoja na mifano katika uwezeshaji wako.
Vitendo vya ujifunzaji Unapoandika vitendo vya ujifunzaji unatakiwa uvichukue ndivyo vitendo vya msingi vitakavyoleta kujengwa ujuzi. Lugha itakayotumika ionyeshe kuwa mtendaji mkuu ni mwanafunzi. Mfano Wanafunzi, kuchora, kueleza,Kujibu maswali ya mwalimu, kujadiliana,kutafsiri,kueleza, kusoma, kujadili, kufupisha n.k
Vifaa/zana Matumizi ya zana katika kujifunzia na kufundishia ni nyenzo muhimu sana kwa sababu inatumika katika ujenzi wa maana kwa kile mwanafunzi atakachojifunza. Vilevile zana humsaidia mwalimu katika kumrahisishia kazi yake ya kufundisha.
Rejea, Mwalimu atapaswa kuonesha vitabu vya rejea katika mada atakayoifundisha, Kumbuka rejea siyo vitabu tu, bali inahusisha vitu vingine kama majarida, magazeti,vipeperushi, vipindi vya redio, kanda za video, chati na makala mbalimbali na intaneti.
Upimaji, katika upimaji tunaangalia ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji uliofanyika katika malengo mahsusi. Upimaji huu unahusu vitendo hivyo vimefanyika kwa kiasi gani kuleta ujuzi. Mfano, mwalimu anaangalia ni jinsi gani vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji vimefanikiwa.
Maoni, Inahusu hatua au ushauri utakaouchukua baada ya kufanya upimaji.
Mfano wa muundo wa azimio la kazi
Jina la mwalimu :………………. Mwaka:………………………..
Shule: …………….. Muhula:…………………………
Somo: ……………… Darasa:……………………………..
Ujuzi
Malengo
mwezi
wiki
Mada kuu
Mada ndogo
vipindi
v/ufundishaji
v/ufundishaji
vifaa/zana
rejea
Upimaji
maoni

MBINU ZA KUFUNDISHA MADA YA NAMBA NZIMA


1.1 Dhana ya Namba Nzima
Muda: Saa 3
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kufafanua dhana ya namba nzima
b) Kubainisha namba nzima
c) Kueleza umuhimu wa namba nzima katika maisha.
2
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bungua bongo ili kupata dhana ya namba nzima.
b) Maswali na majibu kubaini idadi ya vitu mbalimbali
vinavyowakilisha namba nzima.
c) Majadiliano na uwasilishaji.
d) Kufanya ngonjera/igizo.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Vihesabio kama vifuniko vya soda au vifuniko vya maji, kokoto,
vijiti punje za nafaka.
b) Abakasi
c) Kasha la namba
d) Kadi za namba nzima.
Upimaji
a) Maswali ya mdomo.
b) Jaribio.
c) Mazoezi
1.2 Kujumlisha na Kutoa Namba Nzima
Muda: Saa 3
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kufafanua dhana za kujumlisha na kutoa
b) Kujumlisha namba nzima
c) Kutoa namba nzima
d) Kubaini mifano katika maisha inayohusisha dhana za kutoa na kujumlisha
nambaa nzima.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bunguo bongo
b) Onesho mbinu
c) Kazi za vikundi na uwasilishaji
3
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Vihesabio
b) Abakasi
c) Kasha la namba
d) Kadi za namba nzima
Upimaji
a) Mazoezi binafsi
b) Jaribio
c) Kumbukumbu binafsi za mwanafunzi
1.3 Kuzidisha na Kugawanya Namba Nzima
Muda: Saa 3
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) kufafanua dhana za kuzidisha na kugawanya
b) kuzidisha namba nzima
c) kugawanya namba nzima
d) kubaini mifano katika maisha inayohusiha dhana za kuzidisha na
kugawanya namba nzima.
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) KWL na mhadhara shirikishi
b) Onesho-mbinu , michezo, maswali na majibu na majadiliano
c) Kazi za vikundi na uwasilishaji
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Vihesabio
b) Michoro/picha za kuonesha makundi ya vitu
c) Kadi za kuzidisha namba nzima
d) Chati ya kuzidisha namba nzima
e) Kadi za kugawanya namba nzima
4
Upimaji
a) Zoezi binafasi.
b) Fomu ya uchunguzi.
c) Majaribio
1.4 Kigawe Kidogo cha Shirika (KDS) na Kigawo Kikubwa cha Shirika (KKS)
Muda: Saa 5
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kuchanganua dhana za kigawe na kigawo
b) Kuorodhesha vigawe vya namba nzima.
c) Kubaini na kukokotoa Kigawe Kidogo cha shirika (KDS) cha namba
nzima
d) Kutafuta vigawo vya namba nzima na kubaini KKS
e) Kukokotoa kigawo kikubwa cha shirika (KKS) cha namba nzima
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
Onesho mbinu, majadiliano na kazi kwa vikundi katika kutafuta KDS na
KKS.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chati ya kuhesabia.
b) Tebo ya kuzidisha
c) Kadi za viwango
Upimaji
a) Maswali ya mdomo.
b) Zoezi binafsi.
5
2.0 SEHEMU
2.1 Dhana ya Sehemu
Muda: Saa 5
Malengo Mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza dhana ya sehemu
b) Kutofautisha aina za sehemu
c) Kutaja majina mengine ya sehemu
d) Kulinganisha sehemu mbalimbali
e) Kuonesha matumizi ya sehemu katika maisha ya kawaida
Mbinu za Kufundishia na Kujifunzia
a) Bungua bongo
b) Onesho mbinu, maswali na majibu.
c) Majadiliano kwa vikundi.
Zana/Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
a) Chati za sehemu.
b) Kisu, mkasi, karatasi
c) Vihesabio
d) Chaki/kalamu za rangi
Upimaji
a) Tathmini binafsi
b) Zoezi.
c) Jaribio.

YATOKANAYO NA KIKAO CHA WALIMU WAKUU,WARATIBU ELIMU KATA NA MRATIBU WA KITUO CHA WALIMU BUHIGWE CHA TAR 12.08.2012


Tarehe 12.08.2012 kilifanyika kikao cha walimu wakuu wote wa eneo la Cluster ya Buhigwe na Waratibu Elimu Kata na Mratibu wa kituo cha walimu Bhigwe.Jumla ya walimu wakuu 33 na waratibu elimu kata 12 na mratibu Trc walihudhuria kikao hicho. Kikao hicho kilifanya tathmini ya mtihani wa utimilifu wa Cluster ya buhigwe na mambo mengine yanayohusu elimu. Yafuatayo ni yatokanayo na kikao hicho
Washiriki walikubaliana wanunue photocopy machine itakayotumiwa na shule zote hasa katika shule za mitihani , hivyo ilikubaliwa kila shule ichangie shilingi 32,000/= ili kuweza kutimiza sh 2,100,000/= kwaajili ya manunuzi ya Photocopy machine. Fedha hiyo inatakiwa hadi kufikia january 2014 iwe imekusanywa. Pia tulikubaliana kuanza kituo cha walimu kianze kutoa mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa walimu wanaojiendeleza katika vipindi vya likizo. Pia walimu wakuu walikubaliana kuwa wanachangia shilingi 7000 kila mwaka kwa ajili ya malipo ya mlinzi wa kituo cha walimu Buhigwe. Pia kiwango cha uchangiaji kwa ajili ya mtihani wa utimilifu wa TRC kilipandishwa toka sh 3000/= hadi sh 4000/=.

Jumapili, 11 Agosti 2013

Elimu Tanzania tuna mwelekeo sahihi?



 Na Felix Mwakiyembe

CHANGAMOTO kubwa inayoikabili sekta ya elimu nchini ni ubora wa elimu, na hata Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inalitambua hilo ambapo moja ya malengo yake katika kipindi cha miaka 50 ijayo ni kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote.
Ni changamoto ambayo imetokana zaidi na upanuzi mkubwa uliofanyika kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru, kuanzia ngazi ya elimu ya awali hadi ile ya chuo kikuu, elimu ya watu wazima pamoja na ile ya ufundi.
Kutokana na changamoto hiyo, wananchi walio wengi kuanzia wale wa kawaida hadi wana taaluma na hata baadhi ya viongozi wamekuwa wakiamini kwamba hakuna maendeleo yaliyofikiwa kwenye sekta ya elimu tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania Bara miaka 50 iliyopita.
Takwimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinatoa jibu la mkanganyiko huo kwa kuonyesha hali ya elimu nchini ilivyokuwa kabla ya uhuru na ile baada ya uhuru, na ni kwa kufanya ulinganisho wa nyakati hizo mbili ndipo tunaweza kufikia hitimisho la hoja kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Elimu kabla ya uhuru
Nyaraka mbali mbali zilizopo zinabainisha kwamba mfumo wa elimu uliokuwepo kabla ya uhuru ulikuwa ni wa kibaguzi, elimu ilitolewa kwa kuzingatia matabaka ya rangi, ambapo Mwafrika alikuwa ni daraja la mwisho kabisa katika ubora, daraja la tatu, Muasia akawa daraja la pili na Mzungu alikuwa ndiye wa daraja la juu kabisa, la kwanza.
Matabaka haya yalionekana wazi wazi kwenye mpangilio wa shule, mathalani, mwaka 1960, kulikuwa na shule za msingi 3,270 zilizokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 450,626 lakini zikiwa  zimegawanywa kwa kuzingatia rangi ambapo za  Waafrika zilikuwa 3,115 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 431,056, na wasio Waafrika zilikuwa 155 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 19,570.
Mfumo huo wa kitabaka katika utoaji elimu ulikuwepo hata kwenye shule za sekondari ambako nako ilitolewa kwa misingi ya matabaka ya rangi.
Hata hivyo takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu zinaonyesha kwamba kwa elimu ya sekondari ya juu, Waasia na Wazungu hawakusomesha watoto wao hapa nchini bali waliwapeleka kusoma nje.
Mfumo wa elimu kabla ya uhuru uliweka shule ya msingi kuwa ya miaka minne tu, ambayo ni darasa la kwanza hadi la nne. Hata hivyo, kuwepo kwa ada ilikuwa kikwazo kwa wazazi wengi kusomesha watoto, ada ilisababisha nafasi katika shule za msingi na sekondari kutojazwa kutokana na Waafrika wengi kutozimudu.
Elimu ya ufundi stadi waliyopatiwa Waafrika ilikuwa katika daraja la chini kama vile uhunzi, mafundi bomba, fundi seremala, fundi mchundo, rangi, viatu na ushonaji, na mafunzo haya yalitolewa katika shule za Ufundi Ifunda iliyokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 249 na Shule ya Ufundi Moshi iliyokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 390.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa anabainisha kuwepo kwa matabaka kwenye mfumo wa elimu kabla ya uhuru wakati akitoa taarifa ya sekta ya elimu nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri Kawambwa anaongezea akisema kuwa elimu iliyotolewa kabla ya uhuru haikutoa kipaumbele kwa masomo ya sayansi ambayo ni mama wa uvumbuzi, na kwamba hapakuwepo na  chuo kikuu hata kimoja hadi miezi saba kabla ya uhuru kilipoanzishwa  chuo kikuu kishiriki chini ya Chuo Kikuu cha London.
Elimu baada ya uhuru
Mara baada ya uhuru yalifanyika mabadiliko makubwa katika mfumo mzima wa elimu nchini ikiwemo kufuta utoaji elimu kwa kuzingatia matabaka ya rangi.
“Mfumo wa utoaji elimu ulifanyiwa marekebisho ili kupata mfumo unaofaa kurudisha heshima na utamaduni wa Mtanzania na kukidhi mahitaji ya jamii na nchi huru,” anasema Waziri Kawambwa na kuongeza:
“Serikali ilitoa elimu kwa watoto wote bila ubaguzi, muda wa elimu ya msingi uliongezwa kutoka miaka minne hadi nane mwaka 1965 muda wa kusoma Elimu ya Msingi ulipunguzwa na kuwa miaka saba kwa sababu za kifedha.”
Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa ufutaji wa darasa la nane ulifanyika kwa awamu tatu, ya kwanza ikiwa mwaka 1965 ambapo ilihusisha mikoa ya Arusha, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro na Tanga, awamu ya piIi ilikuwa mwaka 1966 kwa mikoa ya Kigoma, Mara, Tabora, Shinyanga, Ziwa Magharibi  na Mwanza na awamu ya tatu ilifanyika mwaka 1967 ikihusu mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya Iringa, Dodoma na Singida.
Lugha ya kufundishia ni miongoni mwa zana muhimu sana katika mchakato mzima wa utoaji elimu, na ni kwa kuzingatia ukweli huo, serikali iliamua lugha za Kiswahili na Kiingereza kuwa lugha rasmi za kufundishia shule za msingi kuanzia mwaka 1964.
Historia ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini inaonyesha kwamba, mwaka 1968, Serikali ilienda mbali zaidi kwa kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kufundishia katika shule za msingi.
Hatua hii ya serikali ni wazi ilizingatia zaidi kanuni zinazotumika kuteua lugha rasmi ya kufundishia, kwamba iwe ni ile inayofahamika na wanafunzi, na kwa Tanzania haikuwa nyingine zaidi ya Kiswahili.
“Kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi kufuata na kuelewa vizuri masomo yao na pia kukuza, kuendeleza na kurithisha utamaduni na Lugha ya Taifa,” anasema Waziri Kawambwa akizungumzia msingi wa uamuzi huo wa serikali.
Hata hivyo, hatua hiyo haikufuta kabisa Kiingereza mashuleni, lugha hiyo ilitumika katika shule za sekondari na vyuo na kwa shule za msingi kilibaki kama somo kwa baadhi ya madarasa.
Maeneo mengine yaliyofanyiwa marekebisho mara baada ya uhuru ni pamoja na kuandaliwa kwa muhtasari wa aina moja kwa nchi nzima ukitilia mkazo kazi za mikono na mambo muhimu ya kukuza umoja na maendeleo ya haraka kwa taifa.
Mwaka 1972, yalifanyika mabadiliko katika mitaala ili kukidhi mahitaji ya taifa, ambapo kutokana na mabadiliko hayo ilianzishwa elimu ya michepuo ya kilimo, ufundi, biashara na sayansi kimu katika elimu ya sekondari ili kutoa stadi za mwelekeo wa kazi, kuoanisha nadharia na vitendo, kuhimiza shule kuzalisha mali kwa madhumuni ya kusaidia kupunguza gharama ya elimu kwa serikali.
Pamoja na michepuo hiyo, ulianzishwa pia mchepuo wa Jeshi la Ulinzi katika shule za sekondari za wavulana na wasichana za Tabora mwaka huo huo wa 1972.
Mwaka 1975 serikali ilifanya maamuzi mengine mazito katika sekta ya elimu kwa kuanzisha Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Wote uliojulika zaidi kama UPE ikiwa ni kifupisho cha mpango huo kwa kiingereza, Universal Primary Eduction, hatua ambayo ilisababisha kupanuliwa kwa  programu za mafunzo ya ualimu.
Kuanzishwa kwa mpango wa kuwachagua wanafunzi kwa kutumia kota za mikoa ili kusaidia kuwapa nafasi sawa watoto kutoka katika maeneo ya nchi yaliyokuwa na maendeleo hafifu kielimu.
Utaratibu mpya wa uteuzi wa wanafunzi kuingia sekondari ulianzishwa ambapo ziliundwa kamati za mikoa za uchaguzi wa kuingia sekondari lengo likiwa kusimamia haki na kutoa nafasi sawa za kuingia sekondari kwa watoto kutoka sehemu zote za nchi.
Mitihani ya Kidato cha pili kufutwa ili vijana wengi zaidi waweze kupata elimu ya sekondari kwa miaka minne badala ya miwili, hivyo kuliwezesha taifa kujipatia wataalamu wake.
Mwaka 1975, serikali ilisitisha mitihani ya kutoka nje ya nchi na kuanzisha Mitihani ya Taifa katika mfumo rasmi wa shule, ili kuokoa fedha za kigeni na kuliwezesha taifa kutathmini mitaala yake kwa misingi ya falsafa ya Elimu ya Kujitegemea.
Karo kwa shule za sekondari za Serikali ilifutwa ili kuwapa fursa watoto wenye sifa lakini waliotoka katika familia zenye vipato duni kuweza kujiunga katika shule za sekondari. Hali hii iliongeza idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule za serikali.
Mwaka 1961, Serikali za Mitaa zilipewa jukumu la kusimamia  shule za msingi na kuundwa  Mamlaka za Elimu za Serikali za Mitaa zilizopewa madaraka ya kuendesha na kusimamia Elimu ya Msingi.
Katika mfumo huo mpya, serikali za mitaa zilichangia  asilimia 40 ya gharama za elimu na serikali kuu  asilimia 60 iliyobaki. Matokeo ya hatua hiyo ni ongezeko kubwa la uandikishaji wa wanafunzi kutoka 486,470 mwaka 1961 hadi 753,114 mwaka 1967.
Mfumo mpya wa elimu ulizingatia vile vile elimu ya juu kwa kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1970, kikiwa cha kwanza hapa nchini, na pia kuweka umuhimu katika elimu ya watu wazima.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu ya Watu iliyoanzishwa mwaka 1961 na Chuo cha Kivukoni kilichoanzishwa mwaka 1963 ndio waliokabidhiwa jukumu la kutoa elimu hiyo wakati huo.
Mafanikio miaka 50 ya uhuru;
Mafanikio katika sekta ya elimu yanajibainisha katika maeneo yote nchini, yakiwemo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ambako sekta hiyo imeweza kuzalisha wataalamu takribani kwenye kila eneo, kama vile watalaamu wa afya, elimu, maji, wahandisi, nishati, madini, hali ya hewa, kilimo, usafiri, sayansi na teknolojia na wengine wengi.
Takwimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonyesha kuwepo kwa mafanikio makubwa kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, ikiwemo ongezeko la shule za msingi kutoka 3,270 mwaka 1961 hadi 16,001 mwaka 2011 (za Serikali 15,412 na za Binafsi 589), huku uandikishaji ukiongezeka  kutoka wanafunzi 486,470 mwaka 1961 hadi 8, 363,386 mwaka 2011.
Mafanikio mengine yanatajwa kuwa ni pamoja na ongezeko la walimu kutoka 9,885 mwaka 1961 hadi 175,449 mwaka 2011 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 1,619.2, huduma za uendeshaji na usimamizi wa shule za awali, asingi, na sekondari zimekuwa karibu zaidi na walengwa kwa sababu ya zoezi la ugatuaji ambalo limeimarisha umiliki wa shule kwa jamii.
Shule za Elimu Maalumu zimeongezeka kutoka nne za wamisionari (Tabora, Buigiri, Irente na Uhuru Mchanganyiko) mwaka 1961 hadi  kufikia 251 mwaka 2011. Aidha, kuna Elimu Jumuishi katika shule zote za msingi. Idadi ya wanafunzi wenye ulemavu imeongezeka kutoka wanafunzi 1,000 mwaka 1960 hadi kufikia 30,433 mwaka 2011. 
Shule za sekondari zimeongezeka kutoka 41 (zikiwemo za binafsi mbili) mwaka 1961, hadi 4,367 mwaka 2011 (za Serikali 3,425 na za binafsi 942), huku uandikishaji wa wanafunzi katika shule ukiongezeka kutoka  wanafunzi 11,832 mwaka 1961 hadi 1,789,547 mwaka 2011, sawa na ongezeko la asilimia 1,5024.6.
Walimu wa shule za sekondari nao wameongezeka kutoka 764 mwaka 1961 hadi 52,146 mwaka 2011, na  uandikishaji wa kidato cha kwanza katika shule za Serikali umeongezeka kutoka wanafunzi 4,196 mwaka 1961 hadi 403,873 mwaka 2011, wakati uandikishaji katika kidato cha tano pia umeongezeka kutoka wanafunzi 236 mwaka 1961 hadi 30,265 mwaka 2011.
Vyuo vya Ualimu vimeongezeka kutoka vitatu, vyote vikiwa vya serikali, mwaka 1961 hadi vyuo 103 mwaka 2011 (vya Serikali 34 na binafsi 69).
Uandikishaji umeongezeka kutoka wanachuo 1,723 mwaka 1961 hadi 37,698 mwaka 2011, na idadi ya wakufunzi imeongezeka kutoka 164 mwaka 1961 hadi 1,833 mwaka 2011.
Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi vimeongezeka kutoka vitatu mwaka 1961 hadi kufikia 912 mwaka 2011 na uandikishaji wa wanafunzi katika vyuo hivyo umeongezeka kutoka wanafunzi 1872 mwaka 1961 hadi kufikia 187,257 mwaka 2011.
Kwa upande wa elimu ya juu, vyuo vikuu vimeongezeka kutoka Chuo Kikuu kishiriki kimoja mwaka 1961 hadi vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki 40 (vya Serikali ni 11 na vya Binafsi 29) mwaka 2011, ambapo uandikishaji umeongezeka kutoka wanafunzi 14 mwaka 1961 hadi 104,130 mwaka 2011.
Idadi ya wanafunzi waliopata elimu ya msingi kupitia Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) iliongezeka kutoka 1,500 mwaka 2001 hadi 185,206 mwaka 2007 na kushuka hadi 82,458 mwaka 2011.
Wanafunzi kupitia mpango huo wa  MEMKWA  waliofaulu na kujiunga na shule za sekondari iliongezeka kutoka 63 mwaka 2001 hadi 2,363 mwaka 2007 na 2,776 mwaka 2011.
Watu Wazima waliojiandikisha katika madarasa ya Elimu ya watu wazima nayo iliongezeka kutoka 600,000 mwaka 1961 hadi 2,059,359 mwaka 1975, lakini hata hivyo  mwaka 2011 ilipungua kufikia 1,050,517.
Hayo ni machache tu katika mafanikio mengi yaliyorodheshwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yaliyopatikana tangu uhuru.
Mbali ya ubora, zipo changamoto kadhaa zinazoikabili sekta  ya elimu nchini ikiwemo kuinua kiwango halisi cha uandikishaji (Net Enrolment Ratio -NER)) katika elimu ya msingi kutoka asilimia 94.0 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia100.
Changamoto zingine nipamoja na kuinua kiwango cha   ufaulu katika ngazi zote za elimu, kuongeza nafasi za wanafunzi wanaojiunga na elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, elimu sekondari ya juu na elimu ya juu.
Kuongeza idadi na kuimarisha rasilimali watu, katika ngazi zote za elimu, kuongeza na kukarabati miundo mbinu ili kukidhi ongezeko la uandikishaji katika ngazi zote za elimu, kuinua idadi ya wananchi wanaoshiriki katika “Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii”.
Kuongeza vitendea kazi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia na mitambo katika ngazi mbalimbali za elimu, kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuwafanya wanafunzi na walimu kuwepo shuleni muda wote, kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji hususani katika masomo ya lugha, hisabati na sayansi, kuimarisha mafunzo kazini endelevu katika ngazi zote za elimu, kuimarisha ukaguzi, ufuatiliaji na tathimini katika ngazi zote za elimu na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ya Wakaguzi wa shule.
Changamoto zingine ni kuimarisha muundo wa uongozi katika kusimamia  utoaji wa elimu bora nchini, kukabiliana na ongezeko kubwa la watu wazima na vijana wasiojua kusoma na kuandika, Kuongeza bajeti ya elimu ili kuweza kutekeleza mipango ya  sekta ya elimu kikamilifu, kuimarisha mawasiliano na wadau katika sekta ya elimu na kuboresha upangaji wa vipaumbele vyenye tija katika sekta ya elimu.
Matarajio ya Wizara kwa Miaka 50 ijayo
Matarajio ya wizara hiyo ni pamoja na kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kutoa visaidizi, vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa watu wenye mahitaji maalum, kuimarisha ufundishaji kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kutoa mafunzo na kuongeza ajira na kupanga waalimu kulingana na mahitaji walimu.
Matarajio mengine ni pamoja na kutoa motisha kwa walimu hasa wale wanaopangwa katika maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi, kupitia na kuboresha mitaala ili iende sambamba na mabadiliko na mahitaji ya nchi na kuimarisha ufundishaji na kujifunza hususan kwa masomo ya hisabati, sayansi na lugha.
Kuongezeka fursa za elimu na usawa kwa kuweka mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga na kukarabati miundo mbinu ya elimu kama maabara, madarasa, maktaba, vyumba vya mihadhara, vyoo na nyumba za walimu na kukamilisha mapitio ya sera ya elimu na mafunzo na mikakati ya utekelezaji wake.
Malengo mengine ni kusimamia ubora wa elimu kwa kuimarisha ukaguzi wa shule, ufuatiliaji na tathmini ya elimu katika ngazi zote za elimu, kuimarisha na kujenga uwezo wa uongozi katika mipango ya elimu na kuimarisha maendeleo ya michezo katika kazi zote za elimu.
Kuandaa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari hususani kwa masomo ya sayansi, hisabati na lugha, kuinua kiwango cha uandikishaji wa watoto wa rika lengwa wa elimu ya msingi kutoka asilimia 95.4 na kufikia asilimia 100 mwaka 2015, kufanya ukaguzi wa shule kuwa wakala wa serikali na kuanzishwa kwa ‘Teachers’ Professional Board’ ili kuinua ubora, umahiri  na maadili ya ualimu.

Makala hii imetolewa kwenye gazeti la Raiamwema la tarehe 9 decemba 2011.